Programu za Simu na Mifumo
Mifumo inayoendesha biashara yako kwa urahisi
Excel na makaratasi yanaposhindwa kwenda na kasi, tunajenga mifumo inayoweza. Kuanzia programu za wateja kwenye Play Store na App Store hadi mifumo ya wafanyakazi, stoo, ankara na booking, tunabuni kulingana na kazi zako halisi za kila siku na kuiunganisha na zana unazotumia tayari.
Inafaa kwa
- Biashara zinazokua
- Wauzaji na wasambazaji
- Usafirishaji
- Shule na vyuo
- Zahanati na maduka ya dawa
- Startups zenye wazo la app
Bei baada ya ushauri wa bure
Unachopata
Kinachojumuishwa kwenye kila mradi
- Kikao cha mahitaji na makubaliano ya maandishi
- Mfano wa muonekano unaobonyezeka
- Programu au mfumo uliojaribiwa
- Kuweka kwenye Play Store / App Store
- Mafunzo na nyaraka
- Mpango wa usaidizi na matengenezo
Teknolojia tunazotumia
Huduma nyingine
Maswali yanayoulizwa mara kwa mara
Inachukua muda gani kutengeneza tovuti?
Tovuti ya Mwanzo huwa tayari ndani ya siku 7 baada ya kupata maudhui yako. Tovuti za Biashara huchukua takribani siku 14 na maduka ya mtandaoni takribani siku 21. Mifumo maalum hupewa muda kwenye makubaliano ya maandishi.
Malipo yanafanyikaje?
Tunaanza na malipo ya awali ya 50% na kiasi kilichobaki hulipwa siku ya kuzindua. Ukipenda, tovuti ya Mwanzo inapatikana pia kwa malipo ya kila mwezi kuanzia TSh 75,000, pamoja na hosting na msaada.
Je, ninamiliki tovuti na domain yangu?
Ndiyo. Domain inasajiliwa kwa jina lako na unamiliki maudhui na muonekano wake. Tunakupa taarifa zote za kuingia na nyaraka wakati wa kukabidhi.
Wateja wangu wanaweza kulipa kwa M-Pesa?
Ndiyo. Tunaunganisha tovuti yako na mifumo ya malipo iliyosajiliwa Tanzania inayopokea M-Pesa, Airtel Money, Mixx by Yas na kadi za benki.
Mnaweza kutengeneza tovuti kwa Kiswahili?
Ndiyo. Tunajenga kwa Kiingereza, Kiswahili au zote mbili. Vifurushi vya Biashara na Duka Mtandaoni vina lugha zote mbili.
Uko tayari kuileta biashara yako mtandaoni?
Tuambie kuhusu biashara yako upate ushauri na bei bure ndani ya siku moja ya kazi.