Ruka hadi maudhui

SEO na Kuonekana Google

Kuwa biashara ambayo wateja wanaipata kwanza

Kila siku watu Tanzania wanatafuta "hoteli Arusha", "spea Kariakoo" au "shule Mbezi". Kama biashara yako haionekani, wateja hao wanaenda kwa mwingine. Tunaweka na kuboresha uwepo wako Google, kurekebisha matatizo ya kiufundi yanayozuia tovuti yako, na kukuletea ripoti rahisi kuelewa kila mwezi.

Inafaa kwa

  • Biashara zenye tovuti lakini wateja wachache
  • Hoteli na waongoza utalii
  • Zahanati, shule na huduma
  • Maduka yanayotaka wateja wa kufika
  • Kampuni zinazolenga Afrika Mashariki

Kuanzia TSh 150,000 / mwezi

Unachopata

Kuweka, kuthibitisha na kuboresha Google Business Profile
SEO ya eneo lako (mji na mtaa)
SEO ya kiufundi: kasi, simu, indexing na structured data
Utafiti wa maneno ya kutafuta soko la Tanzania (Kiingereza na Kiswahili)
Maudhui na makala yanayopendwa na Google
Google Search Console na Analytics
Mkakati wa kupata maoni (reviews) zaidi Google
Ripoti ya kila mwezi: simu, wageni na nafasi Google

Kinachojumuishwa kwenye kila mradi

  • Ripoti ya ukaguzi wa SEO bure
  • Google Business Profile iliyoboreshwa
  • Marekebisho ya kiufundi kwenye tovuti
  • Mpango wa maneno na maudhui
  • Ripoti ya kila mwezi
  • Ushauri wa kweli: hatuahidi nafasi ya kwanza kwa uongo

Teknolojia tunazotumia

Google Search ConsoleGoogle Analytics 4Google Business ProfileSchema.orgLighthouse

Huduma nyingine

Maswali yanayoulizwa mara kwa mara

Inachukua muda gani kutengeneza tovuti?

Tovuti ya Mwanzo huwa tayari ndani ya siku 7 hadi 21 baada ya kupata maudhui yako. Tovuti za Biashara huchukua takribani siku 14 na maduka ya mtandaoni takribani siku 21. Mifumo maalum hupewa muda kwenye makubaliano ya maandishi.

Malipo yanafanyikaje?

Tunaanza na malipo ya awali ya 50% na kiasi kilichobaki hulipwa siku ya kuzindua. Ukipenda, tovuti ya Mwanzo inapatikana pia kwa malipo ya kila mwezi kuanzia TSh 75,000, pamoja na hosting na msaada.

Je, ninamiliki tovuti na domain yangu?

Ndiyo. Domain inasajiliwa kwa jina lako na unamiliki maudhui na muonekano wake. Tunakupa taarifa zote za kuingia na nyaraka wakati wa kukabidhi.

Wateja wangu wanaweza kulipa kwa M-Pesa?

Ndiyo. Tunaunganisha tovuti yako na mifumo ya malipo iliyosajiliwa Tanzania inayopokea M-Pesa, Airtel Money, Mixx by Yas na kadi za benki.

Mnaweza kutengeneza tovuti kwa Kiswahili?

Ndiyo. Tunajenga kwa Kiingereza, Kiswahili au zote mbili. Vifurushi vya Biashara na Duka Mtandaoni vina lugha zote mbili.

Uko tayari kuileta biashara yako mtandaoni?

Tuambie kuhusu biashara yako upate ushauri na bei bure ndani ya siku moja ya kazi.